Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara ashusha waraka ishu ya Rivers kuwa na ukata

MANARA 35454657 1 Manara ashusha waraka ishu ya Rivers kuwa na ukata

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa mhamasishaji wa Yanga SC, Haji Manara, ameshusha waraka mrefu kwenye ukurasa wake wa Instagram, akizungumzia uvumi uliodai kuwa wapinzani wa Yanga kutoka Nigeria, Rivers United hawana pesa.

Huu hapa waraka wenyewe:

Wananchi Ngoja niwastue jambo, juzi na Jana kuna baadhi ya Wachambuzi walitangaza Rivers United wana ukata na huenda wasije kucheza mechi ya marudiano na sisi.

Wengine wakasema wachezaji wao wanne muhimu hawatakuja, Tuliwaelewa dhamira yao, walitaka turelax kisha tuchukulie poa mechi ya marudiano jumapili.

Akili yao wanadhani tutabweteka, kwa uzuzu wao walitaka tuamini mechi ishaisha, Ngoja niwaambie Wapiga Mizinga, @yangasc haijawahi kuamini lolote toka kwao, tunafatilia everything kuhusu Rivers na tunajua kila kitu kuhusu ujio wao.

Yanga hii haiwezi kuingizwa chaka na mazwazwa wanaotaka tusiupe umuhimu mchezo wetu ili baadae waje kutucheka na kutuona mafala, na niwaambie very clear, mnachokiandika na kukisema tunachukulia ni uzuzu tu mlionao.

Rivers wamekuja full Masinondo na Yanga haijawahi na haitawahi kuchukulia mechi ya Jumapili kwa dharau, kisa Kuna Wapiga Ndui wenye njaa zao wamesema.

Tunaendelea na maandalizi yetu Kwa nidhamu na umakini mkubwa, na Insha'Allah tutashinda kisha tutafuzu kwa nusu fainali.

It Iz Wat It Iz, Hii ni Yanga Afrikaaaaaaa, ndimu kawatieni Madunduka, Wananchi tushavuka huko, Bata Wahed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live