Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara amshukia Geoff Lea baada ya kujianika kuwa ni Mwanasimba

Geoff Lea Manara Manara amshukia Geoff Lea baada ya kujianika kuwa ni Mwanasimba

Thu, 18 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amemshukia mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka EFM, Geofrey Lea baada ya mchambuzi huyo kujianika kuwa ni shabiki wa Klabu ya Simba.

Geof ameweka wazi hilio kufuatia comment yake kuonekana kwenye ukurasa wa Instagram wa Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally alipopost picha na kuonesha kuhuzunishwa na maamuzi ya uongozi wa klabu hiyo kuachana na mshambuliaji wao, Moses Phiri raia wa Zambia.



"Haikatazwi kwa mwandishi kushabikia timu flani lakini kujitambulisha kama hivi automatic unakuwa ushapoteza uhalali wa kuaminika na timu nyingine.

"Unaweza kusema au kuandika kitu cha kweli kuhusu Yanga na labda hakitawapendeza washabiki, lakini kwa kuwa usha-declere ufuasi wako wa Makolo, itaonekana una nia mbaya tu.

"Tujitahidi kujizuia hisia zetu kama bado tunaendelea kufanya kazi kwenye media!! Tubaki njia kuu ya Professionalism, ili tupate Legitimacy ya kukosoa na kupongeza both sides," amesema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live