Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara amchamba Fei Toto "Kiko wapi?"

Fei Toto 0001 Fei Toto

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Anaandika Haji Manara baada ya Yanga kubeba ubinhqa qa shiriki;

Makombe yalikuwa sehemu ya maisha yako, mikono yako ilishazoea kubeba Mataji kama haya, uliyabeba sana hadi ukafanana nayo,ulikuwa ukitabasamu hadi tukawa tunaona meno yako yote!! HAYA KIKO WAPI?

Ukakubali kuingizwa Chaka na Wachambuzi Mazuzu na Wakakuaminisha utaendelea kushinda tena na tena Makombe, wakakudanganya na ukawaamini, HAYA KIKO WAP?

Imagine jana ulituziba hadi midomo baada ya kufunga Penaltı yako,hukujipa hata subira Matuta yaishe, unatuletea utoto Wananchi? Ukasusa hadi kuvaa medali yako, unasusa medali SUSAAA,! HAYA KIKO WAPI?

Yanga ni kubwa sana Fei, usithubutu next time kushangilia hadi mechi iishe,Yanga ina Bond na Makombe ya Nchi hii, imeundwa ili ishinde na kushinda na kushinda Mataji ,,ulivyoweka kidole tu kutunyamazisha nikajua tunashinda hi mechi, ulifanya uchuro mkubwa kwa Wananchi, Pole Dogo next time uwe na heshma na adabu kwa Dar Young Africans, HAYA KIKO WAPI?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live