Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema kuwa aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji S Manara alifungiwa na Kamati ya Maadili na si yeye.
Karia amesema hayo baada ya Manara kudai kuwa alifungiwa na TFF kwa chuki binafsi na baadhi ya viongozi wa taasisi hiyo kutokana na umaarufu wake.
“Manara alikuja nyumbani na Engineer Hersi na hata nilivyomfungia alikuja pia, unajua TFF ni taasisi na sio suala la Karia. Haji nimekuta kafungiwa miaka saba (7) watu wanasema ninemfungulia hesabu toka nimeingia miaka saba haijaisha.
“Sina chuki na Haji ni moja kati ya watu niliokuwa nathamini wanachifanya, ingawa kuna sehemu ana mapungufu kama binadamu, ofisi ndio imemshtaki hata alivyokuja nikamwambia siwezi sina mkono wangu.
“Anasema aliniomba msamaha lakini baadae anasema hakufanya kitu namuonea, wewe unaonewaje unaenda kuomba msamaha.
“Kamati ile nimeitengeneza mimi na mkutano wangu mkuu lakini ikishafika kule hata mimi sina mamlaka. Maprofesa wangapi wapo jela! kwanini mpira tu? taratibu zikiwekwa lazima zifuate na adhabu zikitoka lazima zitekelezwe.
“Niulize Haji tangu amefungiwa ametekeleza adhabu? Wangapi wamefungiwa na ni viongozi wakubwa, kila kitu kina mihimili yake mimi ni Rais wa TFF siwezi nikakwambia magoli yamefungwa niyatoe lazima niheshimu taratibu.
“Huyu kafungiwa na kamati ya maadili, ile kamati ya maadili leo nikigusa tu nimekwisha, kwa mfano leo nikisema Haji afunguliwe kesho mtu akinishtaki nimeingilia kamati ya maadili nimekwisha.
“Kwa nini Haji, Wambura kafungiwa maisha mbona hawasemi? Mimi nimeingia ofisini nimekuta rufaa ya Haji nikasema huyu ana haki asikilizwe na akashinda," akasema Karia.