Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara akaa mzunguko

MANARA JANGWANI Manara akaa mzunguko

Sat, 25 Sep 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MSEMAJI wa Yanga, Haji Manara leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ameonekana kukaa katika majukwaa ya mzunguko yofauti na ilivyozoeleka kwa viongozi kukaa jukwaa la VIP.

Manara ambaye alihamia Yanga akitokea kwa wapinzani zao Simba ameingia uwanjano hapo akisindikizwa na mabaunsa wawili kisha kuelekea katika jukwaa la mzunguko alikopokelewa kwa shangwe.

Baada ya kufika pale, Manara alisalimiana na baadhi ya mashabiki kisha kukaa ambapo alionekana kutotulia kwani mashabiki wengi walihitaji kupiga picha naye.

Huu ni mchezo wa kwanza kuzikutanisha Simba na Yanga tangu Manara aihame Simba na kwenda Yanga msimu 2020/2021 ulipo malizika.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz