Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara aishauri TFF fainali ya FA

Haji Manara Sd Manara aishauri TFF fainali ya FA

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara, amelishauri Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusu mchezo wa Fainali ya Kombe la FA kuchezwa Babati, Juni 2, 2024

Mchezo huo utakuwa wa Yanga SC na Azam FC na utapigwa katika Uwanja wa Tanzanite Stadium Babati, Mkoani Manyara.

Manara ameishauri TFF na kuanza kuandika “ NASHAURI TU. Kwa kilichotokea Arusha last weekend kinatupaswa kukifanya kama funzo, Semi final tu Washabiki walimwagika hadi wengine kukosa nafasi ya kuingia Uwanjani na hatimae kusababisha fujo.

“Ikumbukwe ilikuwa ni Sheikh Amri Abedi, Now tunakwenda kwenye fainali yenyewe ya Kombe la Shirikisho, tunaipeleka Babati Manyara, kiwanja chenyewe kina jukwaa moja tu, wataalamu wanasema capacity yake haifiki washabiki elfu tatu hadi elfu nne.

“Mamlaka zetu nawashauri kwa heshma kubwa ondoeni mechi pale kwa kuwalinda Washabiki, Babati ni Centre ya mikoa kadhaa inayoizunguka, Watu watatoka katika mikoa tofauti kuja kuona fainali na Yanga yao.

“Team hii ya Wananchi haijawahi kucheza huko toka iumbwe, imagine hamu ya Wanazi wetu kuiona Team yao, fikirieni na udogo wa uwanja, tunaweza kuepuka maafa kwa kuipeleka fainali sehemu nyingine.

“Kwa sisi watu wa Events na Promotions huwa tunazingatia vitu kadhaa kabla ya tukio husika, FACILITY, CAPACITY, CONIVNENCE NA LOGISTICS. Kwa Tukio kubwa la fainali kupeleka hapo hatukuzingatia mambo hayo.

“Najua pamoja na nia nzuri ya kuusambaza mpira maeneo mengi ya nchi lakini uwanja wa Babati haujawa tayari kuhost fainali hii kubwa, Wenzetu kote duniani fainali ya Makombe kama haya huchezwa katika Main Stadimu ya nchi na hata Mgeni rasmi huwa kiongozi mwandamizi wa nchi.

“Kwa nchi za kifalme lazma aje Royal family kukabidhi kombe. By the way kibiashara pia sio sahihi kama tunataka tuumarket mpira wetu ndani na nje ya nchi, Imagine makampuni makubwa ya nje yakiona fainali katika uwanja kama huu watatuonaje?

“Watapata hamu ya kuja kuinvest kwenye mpira wetu? Nini nafasi ya Azam TV katika eneo la Production? Wanajisikiaje kurusha mechi ya fainali pale? Sponsor CRDB mileage gani watapata kwa fans wachache? Ahhh pengine mawazo yangu leo yanaweza kuwa sio sahihi."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live