Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara aanika kazi yake ndani ya Yanga - Haji Manara

Manara Kamwe Mdz Manara aanika kazi yake ndani ya Yanga - Haji Manara

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Yanga Sc, Haji Manara kupitia Wasafi FM ametaja kazi yake ndani ya Yanga ikiwa ni siku chache baada ya kurejea kutoka kwenye 'kifungo' cha kuzuiwa kujihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kwa miaka miwili.

Manara ambaye amemaliza adhabu yake hivi karibuni ameibua mijadala kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wadhifa wake ndani ya Idara ya Habari ya Yanga ambayo inaongozwa na Ally Kamwe.

“Wakati natambulishwa Yanga Sc Agosti 2021 nilitambulishwa kama Msemaji wa Klabu ya Yanga na Sasa kazi yangu ni ile ile mimi ni Msemaji wa Yanga Sc, kazi yangu ya kimkataba ni kuisemea mabingwa wa kihistoria ya nchi hii.

“Mimi niliajiriwa Yanga kuwa Msemaji wa Yanga, hata mkataba wangu uko very clear, bora uniguse mimi lakini usiiguse Yanga, yani nitaruka na wewe kama Mwewe,” amesema Haji Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live