Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara: Yanga wana nafasi ya kufika Nusu Fainali

Yanga Tizi Geita Manara: Yanga wana nafasi ya kufika Nusu Fainali

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa zamani wa Yanga Sunday Manara amesema Yanga wana faida kubwa ya kufuzu hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga inaanzia ugenini kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Rivers United ya Nigeria, mchezo utakaopigwa Jumapili ijayo.

Manara ambaye ni mchezaji mwenye rekodi kubwa Tanzania amesema wakati walipokuwa wakicheza kimataifa na wakapata fursa ya kuanzia ugenini kwao ilikuwa bahati kwani walikuwa na uhakika wa kufanya vizuri.

Staa huyo wa zamani amezungumza na Mwanaspoti na kusema kuwa Yanga wananafasi ya kuona mbinu zote za wapinzani wao kwa sababu kwao watatoa silaha zote kwani hawatakubali kufungwa uwanja wa nyumbani.

"Wataweza kuwamudu wapinzani wao kwani wanapokuja kucheza nao nyumbani tayari watakuwa wameshafahamu udhaifu wao, naona wana nafasi kubwa ya kwenda nusu fainali;

"Kwa Yanga hii wanaweza kufanya vizuri kwani wataweza kuwamaliza wageni wakiwa nyumbani kiurahisi zaidi kwani hawatakuwa na jipya ila kuzuia wasifungwe,"alisema Manara.

Aliendelea kusema Yanga wanatakiwa kufahamu kuwa watakutana na mashambulizi ya hatari ila watakapokuja nyumbani wapinzani wao watazuia ili wasiweze kufungwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live