Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara: Yanga walistahili kubeba makombe yote msimu huu

Yanga Kombe Mkapa.jpeg Manara: Yanga walistahili kubeba makombe yote msimu huu

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Yanga SC kutwaa kikombe cha CRDB Confederation Cup kwa kuifunga Azam FC jana, Mwanachama wa timu hiyo Haji Manara amesema timu imestahili kushinda kikombe hicho pamoja na kile kikombe cha Ligi Kuu ya NBC walichokitwaa Mwezi uliopita.

Manara amesema msimu huu, Yanga SC walikuwa na timu bora kulinganisha na timu zote za Tanzania na kuongeza iwe unataka au hutaki.

“Iwe unataka au hutaki, huo ndio ukweli ni watu ambao hauishi mpaka uishe ukichanganya na kujituma kwao uwanjani (Fighting Spirit) kiasili Yanga SC ni wapiganaji.

“Ukichanganya ubora wachezaji walionao na mipango ya benchi la ufundi na viongozi tulistahili kushinda vikombe hivi viwili “ alisema Manara.

Manara aliongeza kuwa kikosi hicho msimu ujao kitashiriki Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika na kusema msimu huu walitakiwa kucheza Nusu Fainali, lakini wakatolewa katika robo fainali kwa mbinde.

“Yanga SC tunapaswa kutengeneza kikosi chenye wachezaji wazuri watakaocheza na timu yoyote Barani Afrika, ukiangalia timu zenye mataji makubwa wanakua na kikosi imara, hiko ndiyo tunapaswa kukifanya.

"Tunapaswa kuongeza kikosi kwa wachezaji wenye ubora level ya Ibrahim Bacca, Stephane Aziz KI, Pacome Zouzoua, Khalid Aucho tuwe na wachezaji walau 20 wenye ubora kwa kuwa na kikosi cha uhakika,” alisema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live