Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara: Yanga hata ikipata sare kwa Medeama poa tu!

Manara Bingwa Manara: Yanga hata ikipata sare kwa Medeama poa tu!

Fri, 8 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Msemaji wa Yanga SC, Haji Manara amesema kuwa anayo matumaini makubwa ya timu yake kupata ushindi ugenini katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama FC utakaopigwa leo Kumasi nchini Ghana.

Manara amesema kuwa, hata kama ikitokea wasipate ushindi, yeye hana presha kwa vile ndiyo soka lilivyo huku akiombea angalau wapate hata sare itatosha kwa ajili ya kupiga hesabu ya mechi zijazo.

"Tunahitaji sana ushindi kesho (leo) pale Kumasi tutakapokuwa tukienda kucheza na FC Medeama ya kule nchini Ghana, lakini mimi binafsi hainipi presha ikitokea vinginevyo.

"Tutashukuru na kufurahi sana tukipata alama tatu away, lakini tutasema asante Mungu ikitokea hata sare, ingawa najua tunao Wachezaji wakubwa wanaoweza kushinda.

"Labda kwa nini nasema tukipata hata droo is not bad, ni namna mwenendo wa Group letu jinsi lilivyo, mathalan ikitokea hivyo kisha tukaja kupata matokeo home kwenye Mechi ya Marudiano, tutakuwa na alama tano huku wenzetu wakibakia na alama zao nne.

"Na wale Waarabu wakagawana points Tatu Tatu maana yake tutakapokuwa tukiwakabili Waalgeria kwa mkapa, ni mechi ya Do Or Die tukishinda tu itakuwa tunaelekea kutoboa na hasa kama Ahly atakuwa amepata Points nyingi na Waarabu wenzao pamoja na mechi yao na Medeama.

"Ni hesabu tu na football ipo hivyo, nzuri zaidi ni alama sita dhidi yao na InshaAllah inawezekana," amesema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: