Aliyekuwa msemaji wa Klabu wa Yanga, Haji Manara ametangaza kuacha rasmi kuishabikia Timu ya Manchester United ya nchini Uingereza kutokana na timu hiyo kuwa na mwendelezo wa kupata matokeo mabaya.
Manara amesema hayo mara baada ya Manchester United kupokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabibgwa Ulaya, usiku wa kuamkia juzi.
"Mimi Haji Sunday Ramadhani Manara leo tarehe 13 Desemba, 2023 kwa hiyari yangu na bila kushurutishwa na mtu yoyote wala kushawishiwa, nimejitoa rasmi kuwa shabiki wa Manchester United.
"Kwa sasa ukiachana na Yanga, sina timu yoyote duniani nnayoishabikia, nitabakia kushangilia mpira mzuri tu. Msinihusishe kwa utani au kwa vyovyote vile na Manchester, vinginevyo Glazier na familia yake pamoja na huyo kipara watupishe.
"Mpira hauwezi kunikosesha raha kila siku, Manchester sio baba yangu wala mama yangu na wala sio Zaiy :Lissa useme ntakosa Nyandindu," amesema Manara.