Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara: Simba na Yanga tupangwe kundi moja CAFCL

Manara Kauli Yake Manara: Simba na Yanga tupangwe kundi moja CAFCL

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema anatamani kuona Klabu yake hiyo ikipangwa kundi moja na watani zao wa jadi, Simba SC kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

kauli hii ya Manara inakuja baada ya Simba na Yanga zote kwa pamoja kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo ambapo yanga iliitoa Al-merrikh ya Sudan huku Simba wakiwatoa Power Dynamos ya Zambia.

Manara amesema anatamani mchezo huo na kusema watawafunga mabao 10 kutokana na Simba SC jinsi wanavyocheza sasa.

“Natamani tukutane nao katika hatua hizi za makundi na kwa timu yao jinsi ilivyo tutawafunga idadi kubwa ya mabao. Timu yao inacheza kitoto sana, licha ya kuwa na wachezaji mahiri,“ alisema Manara.

Ikumbukwe kuwa, Simba ipo pot namba 2 wakati Yanga Sc wakiwa pot namba 3, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa miamba hao wa soka Tanzania kukutana kwenye hatua hiyo ambapo droo ya kupanga makundi itafanyika Ijumaa ijayo, Oktoba 6, Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: