Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara: Simba mmelidhalilisha Taifa, bora mpigwe viboko

Haji Manara Mazembe Haji Manara

Sun, 19 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amewajia juu baadhi ya wachambuzi wa soka nchini akiwataka kufuta kauli yao ya kwamba Yanga wanapaswa kuiga uchezaji wa Simba katika mechi za kimataifa.

Kauli hiyo ya Manara ameiandika asubuhi ya leo Jumapili, Februari 19, 2023 ikiwa ni saa chache kufuatia kipigo alichokipa mtani wao wa jadi Simba Sc akiwa nyumbani cha bao 3-0 kutoka wa Raja Casablanca katika mchezo wa mkondo wa pili wa mechi za makundi Klabu Bingwa Afrika.

"Tumetukanwa sana, tumedhalilishwa sana na tumefedheheshwa mno mitandaoni hususan na hawa wachambuzi Wapuuzi wapuuzi nchini.

"Lugha ya kwamba eti tunapaswa kuwaiga Makolo inapaswa kukomeshwa leo, ikome na tusiisikie tena kwenye Taifa hili. May be kama kuwaiga, labda kutembea na basi kinyume nyume nyumba ya pili tu. Toka ninapoishi mini (Hotel Elements Masaki) walipokuwa jana hadi kwa Mkapa walipopakatwa tatu.

"Lugha za aina hii za kututaka eti tuwaige Madunduka haziwaumizi mashabiki peke yao, bali zinawafadhaisha sana Wachezaji wetu. Na leo ndio nafasi yao ya kuiambia Afrika, hii ndio Yanga na hii ndio Official Football Club ya nchi hii!!

"Hii mambo ya kupeana promo za mitandaoni na magazetini wakati wakiingia uwanjani ni Uharo mtupu, zinatakiwa zikomeshwe leo, wachezaji wetu hii ndio nafasi yenu, mkaiarifu Afrika, nchi hii YANGA ndio Mwamba.

"Yes, tunajua Mazembe ni Club kubwa Afrika na ina wachezaji bora, but leo ni lazma Our Players wa-prove wao ni bora kuliko hata neno lenyewe la ubora, wacheze sio tu kwa ajili ya points 3, bali kwa ajili yao na kwa heshma ya Club hii kubwa zaidi Afrika Mashariki,,

"Full Concentration,100 % Marking, focus na kuamini kwenye mentality ya ushindi, hii ndio game ya kuprove ipi team ya mitandaoni, na ipi team ya soccer, team Domo Kaya na Team ya Football, Team Chupli na Team Kweli kweli.

Nb:: Mh Rais kawaahidi Mzigo, mmeenda kulitia aibu Taifa, bora mpigwe viboko tu Makolo,,Bata wahed."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live