Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Sunday Manara amewaponda waliokuwa wakisema kwamba mshambuliaji wa Yanga raia wa Congo DR, Fiston Mayele amegoma kuongeza mkataba kwa kile kilichoelezwa kuwa anataka kumalizia mwaka mmoja uliosalia aondoke klabuni hapo.
Manara amefunguka huku akiwanga watu hao ikiwa ni saa chache baada ya Mayele kutangazwa kuwa ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuwatumikia Wananchi mpaka mwaka 2014.
Mayele alikuwa akiwaniwa na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini, Al Hilal ya Sudan na Wydad Casablanca ya Morocco.
Manara ameandika; "Hivi yule shakunaku aliyekaa Studio na huku mitandaoni na kusema Mayele yupo Yanga kwa mkopo na Tayari anaenda Kaizer, anajisikiaje hivi sasa?
“Halafu alivyo muongo sasa eti kaongea na Rais wa hiyo Club. Nimegundua wenzetu wana mtandao wa Wanaharakati na Wachambuzi wachache wanaowalipa ili kuwapamba na kujaribu kuivuruga Yanga, bud luck inakuwa very temporary, mwisho wa siku uhalisia unashinda.
“Uzuri wa watu wa football nchini wakiwaona tu wanajua, hawa wanalipwa, ila kinachoniuma ni malipo yenyewe sasa, imezidi laki. Mtu unaenda kuongopa hadharani Mayele anaondoka na yupo kwa loan Yanga, sasa utawaambia nn watu? Hizo laki laki si mje kuchukua kwangu tu mseme ya ukweli?" amesema Manara.