Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara: Poleni Vilabu Mtakaoathirika na Kujitoa kwa GSM, Mchawi Wenu Mnamjua

Manaraaaa Manara: Poleni Vilabu Mtakaoathirika na Kujitoa kwa GSM, Mchawi Wenu Mnamjua

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Kampuni ya GSM kutanga kujitoka kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu ya NBC 2021/22 kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni matakwa ya mkataba kutotimizwa kwa upande wa TFF na Bodi ya Ligi.

Msemaji wa Klabu ya Yanga @hajismanara Kupitia ukarasa wake wa Instagram ametoa pole Kwa vilabu vyote vilivyoathirika na uamuzi huo wa GSM.

“Najua hayakuwa maamuzi mepesi kwa Kampuni, lakini nini GSM ingefanya zaidi ya ilichoamua?

"Haiwezekani masharti ya Mkataba yakiukwe kwa maksudi kisha hakuna hatua zilizochukuliwa siku zote, bado Mtu aendelee kupoteza pesa zake!

"Poleni Vilabu vyote vilivyoathirika na uamuzi huu, lakini Mchawi wenu mnamjua. Wenye akili tunakuunga Mkono 100%,” ameandika Hajis Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live