Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara: Ngoma ni bonge la kiungo

Ngoma Pics Fabrice Ngoma.

Sun, 19 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Afisa Mhamasishaji wa Yanga,Haji Manara amesema kuwa Kocha Robertinho Oliveira alikua anakosea kumpanga Fabrice Ngoma katika eneo la kiungo cha ukabaji wakati kwa uhalisia Midifield Teacher ni kiungo ambaye uwezo wake ni kuchezesha timu na si mtu wa kazi chafu.

Manara amemtaja Ngoma kuwa ni fundi kweli wa mpira,na huwa anaonekana zaidi pale timu inavyoshambulia,inao mpira,lakini Simba inapokutana na timu kama ya Yanga,Ngoma anaonekana dhaifu!

Amesema Ngoma alipokutana na Khalid Aucho na Mudathir Yahya ambao kiasili ni wakabaji,wakatili na hawatoi nafasi ya kufanya jambo lako kiurahisi,lazima aonekane wa kawaida ikizingatiwa anachezeshwa katika eneo lisilo lake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live