Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara: Mama yangu alinizuia kukata rufaa CAS

Manara Kariaaa Manara: Mama yangu alinizuia kukata rufaa CAS

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema kuwa familia yake ilimzuia kukata rufaa kwenye Mahakama ya Usuluhishi wa Masuala ya Michezo (CAS) baada ya kufungiwa na Kamati ya Maadili ya TFF kujihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miaka miwili.

Manara amemaliza adhabu yake aliyofungiwa kujihusisha na mpira ndani na nje ya nchi. Manara alifungiwa miaka miwili pamoja na faini ya milioni 10 baada ya kukutwa na hatia ya kumkosea nidhamu Rais wa TFF, Wallace Karia.

Manara aliyekuwa ameambatana na familia yake kwenye kikao hicho amesema sambamba na kutumikia 'kifungo cha soka' cha miaka miwili pia amelipa faini ya shilingi milioni 10 za Tanzania iliyokuwa imeambatanishwa kama sehemu ya adhabu yake.

"Kwanza kabisa niwashukuru wote kwa kipindi cha miaka miwili niliyofungiwa, na kwa hili nipeleke shukrani zangu za dhati kwa familia yangu hususani mama yangu.

"Wakati nafungiwa kuna watu waliniambia nikate rufaa CAS lakini mama yangu akaniambia miaka miwili sio mingi nisikate rufaa na kweli miaka miwili imeisha na leo niko hapa kuzungumza na watu wa mpira," amesema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live