Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara, Bumbuli midomo yawaponza, wakutana na rungu la Adhabu

Yanga Wacharukaq wahanga wa Adhabu Yanga

Fri, 11 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafisa Habari wa Yanga, Haji Manara na Hassan Bumbuli wamepigwa faini ya Shilingi za Kitanzania Laki tano (500,000) kila mmoja kwa kosa la kuwashutumu waamuzi wa Ligi Kuu kupitia Vyombo vya Habari.

Manara na Bumbuli walizungumza na Wanahabari Februari 8, kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Klabu ya Yanga na kwa mujibu wao walidai wanakumbusha tu waamuzi kutekeleza majukumu yao wawapo viwanjani.

Manara na Bumbuli walizungumzia mambo mbali mbali ikiwemo nyongeza ya muda baina ya mechi za Simba na Yanga.

Sasa kamati ya uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania wametafsiri malalamiko hayo kuhusishwa na kwamba waamuzi wanapendelea baadhi ya timu na kwa mujibu wa sheria namba tano (5) ya mpira wa miguu kamati hiyo imesisitiza mtunza muda ni mwamuzi pekee katika mechi.

Mbali na Faini, Kamati hiyo imetoa onyo kali kwa wote wenye tabia ya kuhoji suala la muda wa nyongeza katika mechi za Ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live