Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara: Bodi ya Ligi wamlipe Pacome

Pacome Zouzoua Nov.jpeg Manara: Bodi ya Ligi wamlipe Pacome

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema kuwa bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara wanapaswa kumlipa pesa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Peodoh Pacôme Zouzoua.

Manara amesema hayo akidai kuwa uwezo anaouonyesha mchezaji huyo Raia wa Ivory Coast kwenye Ligi ya Tanzania ni mkubwa na anaipandisha thamani ya ligi hiyo.

Pacome amesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea ASEC Mimosas na amekuwa mhimili mkubwa kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Miguel Gamondi.

"Mbali na pesa ambayo Al Nassr wanatoa kumlipa Ronaldo katika Ligi ya Saudi Arabia, lakini chama cha mpira cha pale kinatoa fedha kumlipa Ronaldo kwa kuwa ameenda kuongeza kitu katika mpira wao. Mtu kama Pacome huyu ni hatari. TFF, TPLB zimlipe. Anafanya vitu vikubwa sana," amesema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: