Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man Utd yatangaza dau la Harry Maguire

Harry Maguire After Man Utd Concede A Goal Harry Maguire

Tue, 11 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchester United imeweka wazi kiwango cha fedha inachokitaka kwa ajili ya kumuuza Beki Harry Maguire, ambacho kinaweza kuwa kikwazo kwa timu zinazomhitaji kutokana na kuwa juu.

Mchezaji huyo mwenye miaka 30, alisajiliwa na Mashetani Wekundu 2019 kwa ada ya uhamisho ya Pauni 60 milioni, ikiwa ni rekodi, ikiwa ni rekodi ya usajili kwa uhamisho wa beki.

Hata hivyo, alianza katika michezo 16 pekee msimu uliopita, nusu ikiwa ya Kombe la FA na Kombe la Ligi, wakati nahodha huyo akipoteza namba kikosini chini ya kocha Erik ten Hag, na Gazeti la Mall Sport limeandika kuwa ni miongoni mwa watakaouzwa.

Mtandao wa Manchester Evening News umeripoti kuwa Manchester United imeweka kiasi cha Pauni 50 milioni kwa timu takayomtaka Maguire.

Nyota huyo wa kimataifa wa England amebakiza miaka miwili lakini inavyoonekana klabu imeamua kumuweka sokoni akikosa nafasi mbele ya Ten Hag.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: