Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man Utd 'moja ya timu zinazoburudisha' ligi ya Premia - Ten Hag

Man Utd 'moja Ya Timu Zinazoburudisha' Ligi Ya Premia   Ten Hag Man Utd 'moja ya timu zinazoburudisha' ligi ya Premia - Ten Hag

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anaamini kuwa timu yake ni mojawapo ya waburudishaji wakubwa wa ligi ya Premier kwa sasa, ingawa wanatatizika kushinda mechi.

United walitoka sare ya 1-1 na Burnley walioshika nafasi ya pili Jumamosi baada ya mlinda lango Andre Onana kusababisha penalti ya dakika za lala salama iliyomruhusu Zeki Amdouni kusawazisha mkwaju huo.

Ina maana vijana hao wa Ten Hag wameandikisha ushindi mmoja pekee ndani ya dakika 90 tangu katikati ya mwezi Machi na wamechukua pointi saba kutoka kwa mechi sita zilizopita za ligi.

Kwa jumla, kumekuwa na mabao 38 yaliyofungwa katika mechi nane zilizopita za United.

"Sisi ni mojawapo ya timu zenye nguvu na burudani katika ligi kwa wakati huu," Ten Hag aliambia BBC Mechi ya Siku.

Chanzo: Bbc