Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man Utd mdogo mdogo kwa Lautaro Martinez

Lautaro Martinez Cropped A0zlnp4jg3pf1hwdhbuubht6c Lautaro Martinez

Sat, 13 May 2023 Chanzo: Dar24

Klabu ya Manchester United imeripotiwa inamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayekipiga Inter Milan ya Italia, Lautaro Martinez, ili iweze kumsajili wakati wa majira ya Kiangazi.

Martinez amekua akionyesha ubora mkubwa ndani ya Inter Milan kwa muda mrefu sasa, huku United wao wakiwa wanatafuta Mshambuliaji mwenye ubora mkubwa ili kuboresha safu yao ya ushambuliaji.

United imekua ikitafuta mshambuliaji wa kiwango cha dunia kwa muda mrefu na wanahusishwa na washambuliaji kadhaa kama Harry Kane anayekipiga Tottenham.

Lakini inaelezwa hofu yao kubwa ni huenda wasimpate mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England kutokana na ugumu wa bosi wa klabu hiyo, Daniel Levy na sasa wamemgeukia Lautaro.

United iliyoko chini ya kocha Erik Ten Hag inataka kutengeneza timu yenye ushindani mkubwa na kuirudisha kwenye ubora wake.

Mbali na United, Laurato ameshahusishwa na klabu kadhaa kubwa duniani kutokana na aina yake ya uchezaji wake.

Chanzo: Dar24