Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yawataka Cunha, Kudus kwa mpigo

Skysports Mohammed Kudus West Ham 6293264 Mohammed Kudus

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Manchester United imepanga kutumia Pauni 60 milioni kwenye usajili wa straika wa Wolves, Matheus Cunha huku ikiweka mipango yake sawa, kumnyakua pia supastaa wa West Ham United, Mohamed Kudus ambaye amekuwa kwenye ubora wa hali ya juu msimu huu.

Straika Cunha kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na Man United tangu alipokuwa Atletico Madrid kabla ya kwenda Wolves na huenda akabadili timu kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi baada ya hivi karibuni kusema kuwa anataka kupata changamoto nyingine.

Hata hivyo, imekuwa ikielezwa kuwa staa huyo anataka kucheza kwenye michuano ya Ulaya msimu ujao na nafasi hiyo anaweza kuipata endapo atajiunga na Man United.

United inahitaji saini ya Cunha kama atakuwa anapatikana sokoni kwa sasa, huku Kudus akiwemo kwenye orodha ya mastaa ambao timu hiyo inataka kwenda nao kwenye maandalizi ya msimu mpya.

Kudus mwenye miaka 23 amefunga mabao 14 kwenye michezo 44 aliyoichezea timu hiyo ya London.

Winga huyo wa zamani wa Ajax amekuwa na uhusiano mzuri na Meneja wa Man United, Erik ten Hag na inaonekana kuwa ushawishi wa kocha huyo unaweza kumfanya akalazimisha dili la kujiunga na United. Cunha mwenye miaka 25 akiwa na Wolves amefunga mabao 12 kwenye Ligi Kuu England na kuasisti mara nane msimu uliopita, akiwa mmoja kati ya wachezaji ambao walionyesha kiwango cha juu kwenye timu hiyo.

ARSENAL imeripotiwa kuwa na mpango wa kumpiga bei straika wake Eddie Nketiah kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. Fowadi huyo anapendwa sana na kocha Mikel Arteta, lakini hapati nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza. Na sasa, Nketiah atashushwa na kuwa chaguo la chini zaidi kwenye kikosi hicho cha Arsenal. Timu za Fulham na Crystal Palace zinahitaji saini yake.

BEKI wa Barcelona, Ronald Araujo ameripotiwa kwamba atasubiri kuona ni kitu gani kitafuata baada ya jina lake kuhusishwa kwenye mpango wa kubadili timu kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. Bayern Munich na Manchester United zinaripotiwa kuhitaji saini ya supastaa huyo wa kimataifa wa Uruguay, huku kila moja ikipanga kunasa saini yake kwenye dirisha hili.

ATLETICO Madrid inaripotiwa kuwa na mpango wa kunasa saini ya beki wa kati wa West Ham United, Nayef Aguerd kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi. Atletico imetenga Pauni 20 milioni pamoja na bonasi nyingine ili kumvuta beki huyo. Mkali huyo wa kimataifa wa Morocco ameonekana kuwa tayari kwenda kucheza soka Hispania kwa ada ya Pauni 30 milioni.

STAA, Paolo Dybala ameripotiwa kuwamo kwenye orodha ya wachezaji wanaosakwa na kocha Jose Mourinho kwa ajili ya kwenda kufanya nao kazi huko Fenerbahce kuanzia msimu ujao. Mourinho alichaguliwa kuwa kocha mpya wa miamba hiyo ya Uturuki hivi karibuni, hivyo tayari ameweka majina ya wachezaji watatu anaotaka wasajiliwe akiwamo supastaa huyo wa Kiargentina, Dybala. Staa wengine kwenye orodha hiyo ni Romelu Lukaku na Anderson Talisca.

KIUNGO, Luka Modric amesema kwamba yupo kwenye hatua za mwisho kukamilisha mpango wa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Real Madrid. Staa huyo wa kimataifa wa Croatia mkataba wake wa sasa utafika tamati mwishoni mwa msimu huu dili jipya lipo mezani na muda wowote anaweza kusaini. Amekuwa mwenye furaha baada ya Real Madrid kunyakua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa. Ulaya mwaka huu 2024.

KLABU za Ligi Kuu England zimepanga kuvamia kwenye kikosi cha Luton Town kwenda kunasa mastaa kadhaa akiwamo Teden Mengi. Ripoti zinafichua kwamba ukiweka kando timu za England, mabingwa wa Bundesliga, Bayer Leverkusen wamekuwa kwenye mchakato huo, huku Mengi akionekana kuwa mchezaji anawindwa na timu nyingi kutokana na kiwango chake.

KLABU za Ligi Kuu Marekani zinaripotiwa kuhitaji huduma ya mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann baada ya kutambua kwamba saini yake inaweza kupatikana kwa ada ya Pauni 12.8 milioni tu kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi. Griezmann ameonyesha kiwango kizuri msimu wa 2023-24 alipofunga mabao 24 na kuasisti mara nane.

Chanzo: Mwanaspoti