Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yatinga robo Fainali Carabao Cup

United Vs Burnley E1671667208863 1200x640 Man United yatinga robo Fainali Carabao Cup

Thu, 22 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United imefanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la Carabao kufuatia kuibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Burnley katika mchezo uliochezwa uwanja wa Old Trafford Jumatano.

Magoli ya Manchester United yamefungwa na Christian Eriksen akimalizia pasi nzuri ya Aaron Wan-Bissaka dakika chache kabla ya mapumziko kisha Marcus Rashford akafunga bao binafsi baada ya kupokea pasi ya Scott Mctominay.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kufuzu robo fainali ambapo kwenye mechi hiyo takribani wachezaji watano wa Manchester United walishiriki fainali ya Kombe la Dunia Qatar 2022 akiwemo Rashford.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live