Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yashinda kibabe, Ronaldo hazuiliki

JiI SuiP Mfungaji wa goli la ushindi, Cristiano Ronaldo

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashetani wekundu,timu ya Manchester United imetoka nyuma na kushinda 3-2 dhidi ya Atalanta katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.

Atalanta ilitangulia kwa mabao ya Mario Pasalic dakika ya 15 na Merih Demiral dakika ya 28, kabla ya Man United kuzinduka kwa mabao ya Marcus Rashford dakika ya 53, Harry Maguire dakika ya 75 na Cristiano Ronaldo dakika ya 81.

Kwa ushindi huo, Man United ya kocha Mnorway, Ole Gunnar Solskjaer inafikisha pointi sita na kupanda kileleni Kundi F ikizizidi pointi mbili kila moja, Atalanta na Villarreal, wakati Young Boys yenye pointi tatu inashika mkia baada ya mechi tatu.

Matokeo hayo huenda yakapunguza presha kwa Mwalimu wa United Ole Gunnar Solkjaer kutokana na kulalamikiwa kutofanya vyema kwa kikosi chake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live