Sina shaka kwamba hata wapenzi na mashabiki wake kwa sasa hawapendi kuiona ikicheza kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya wanayoyapata na hata aina yao ya uchezaji.
Ndicho unachoweza kusema kwa sasa juu ya kikosi cha Man United baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-0 nyumbani Old Trafford huku wakionesha kiwango dhaifu kabisa mbele ya Mahasimu wao Man City.
Mabao ya Erick Bailly aliyejifiunga dakika ya saba na Bernardo Silva dakika ya 45 baada ya makosa ya kizembe yaliyofanywa na walinzi wa United,yalitosha kuipa ushindi Manchester City wa 2-0 dhidi ya wenyeji.
Manchester City ilitawala sehemu kubwa ya mchezo huo na kama sio uhodari wa mlinda mlango David De Gea huenda hali ingekua mbaya zaidi.
Man City inafikisha pointi 23 na sasa inazidiwa pointi nne na vinara, Chelsea wakati Man United inabaki na pointi zake 17 katika nafasi ya tano.
Jambo kubwa linalotazamiwa na Mashabiki wa Man United kwa sasa ni kuona Koca wa kikosi hicho anafungashiwa virago kwani wengi wanaamini hana uwezo wa kufundisha klabu hiyo.