Manchester United imepewa nafasi ya kumsajili straika wa Benfica, Goncalo Ramos, 21, katika dirisha hili la usajili barani Ulaya ikiwa itaweza kulipa Pauni 80 milioni ambazo ndizo kiasi cha fedha cha bei yake kwa sasa.
Ramos ambaye alionyesha kiwango bora kwenye michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Qatar mwishoni mwa mwaka jana, ambapo alifunga mabao matatu (hattrick) kwenye mchezo dhidi ya Uswisi.
Mkataba wake unatarajiwa kumalizika ifikapo 2026 na msimu uliopita alicheza mechi 47 za michuano yote na kufunga mabao 27, huku akitoa asisti 12.
Man United imekuwa ikihangaika kutafuta straika ambaye atakwenda kuboresha eneo la ushambuliaji ambalo kwa msimu uliopita halikuwa na takwimu nzuri. Mara kadhaa imejaribu kutaka kumsajili Victor Osimhen, lakini changamoto imekuwa ni kiasi kikubwa cha pesa ambacho Napoli inakihitaji ili kumuuza.