Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yamganda fundi wa Kireno

Joao Neves Jõao Neves

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mmiliki mpya wa Manchester United, tajiri Sir Jim Ratcliffe amepania kukifanya kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Old Trafford kuwa cha kibingwa na kurejesha makali yake ndani ya muda mfupi ujao.

Bilionea huyo wa Uingereza anamiliki asilimia 25 ya hisa za Man United baada ya kuzinunua kutoka kwa wamiliki wakuu wa timu hiyo, familia ya Glazer kwa mkwanja mrefu.

Tajiri Ratcliffe uwekezaji wake kwenye kikosi cha Man United utazingatia zaidi kwenye masuala ya kisoka na huko kipaumbele kitawekwa kwenye usajili wa mastaa wapya.

Katika jambo hilo, kwa mujibu wa taarifa za kutoka Ureno, mmoja wa wachezaji ambao tajiri Ratcliffe ni mkali wa Benfica, Joao Neves.

Kocha, Erik ten Hag naye ameripotiwa kuvutiwa na kiunga huyo mwenye kipaji kikubwa, ambaye wakala wake ni Jorge Mendes.

"Rais wa Benfica, Rui Costa ndiye mwenye uamuzi wa mwisho," alisema Mendes alipoulizwa juu ya uwezekano wa kinda huyo kupigwa bei kwenye dirisha hili.

"Yeye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kwenye klabu. Ataamua akubali maombi na kwa masharti gani."

Mendes alipoulizwa kama Benfica imepokea ofa yoyote ya kuhusu mchezaji huyo, alisema: "Ndiyo, vitu kama hivyo havikwepeki hasa ikizingatiwa milango ipo wazi. Mchezaji mwenyewe bila shaka atabaki hadi mwisho wa msimu, baada ya hapo sijui nini kitafuata, Rui Costa ataamua."

Chanzo: Mwanaspoti