Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yalazimishwa sare na Leeds United, Rashford bado wa moto

Man Utd Vs Leeds.jpeg Mchezo ulimalizika kwa United kutoka nyuma na kusawazisha mabao yote mawili

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United wakiwa nyumbani wameshindwa kufurukuta mbele ya Leeds United kwa kupata sare ya bao 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la Old Trafford.

United walilazimika kutokea nyuma kwa magoli mawili na kutoa sare hiyo baada ya timu iliyobila kocha Mkuu Leeds kuongeza mapema kipindi cha kwanza kupitia kwa Wilfried Gnonto kabla ya ungwe ya pili pia kuongeza bao la pili na mlinzi wa kifaransa Raphael Varane akajiweka kambani.

Mabao ya mashetani wekundu yamefungwa na Marcus Rashford kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi iliyopigwa na Diogo Dalot kabla ya Jadon Sancho kufunga bao la pili na la kusawazisha.

Leeds United ilimtimua aliyekuwa kocha wake Jesse Marsch siku ya Jumatatu ambayo imewasaidia kuvuna alama moja ambayo siyo sawa na kiwango ambacho walikuwa wanakionyesha chini ya mwalimu huyo.

Timu hizo mbili zitarudiana tena siku nne zijazo kwenye mechi nyingine ya Ligi raundi ya pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live