Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yalazimishwa sare Old Trafford

IMG 0008.jpeg Man United yalazimishwa sare Old Trafford

Sat, 27 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Manchester United wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Burnley FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.

Mshambuliaji Mbrazil, Antony Matheus dos Santos alianza kuifungia Manchester United dakika ya 79, kabla ya mshambuliaji Mswisi mwenye asili ya Tunisia, Mohamed Zeki Amdouni kuisawazishia Burnley kwa penalti dakika ya 87.

Kwa matokeo hayo, Manchester United inafikisha pointi 54 katika nafasi ya sita ikiizidi tu pointi moja Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 34, wakati Burnley inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 35 nafasi ya 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live