Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yakamilisha usajili wa Gilikipa mwingine

Bandir Altay Bayindir

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kukamilisha usajili wa golikipa mwingine kutoka nchini Uturuki Altay Bayindir ambaye alikua anakipiga klabu ya Fenerbahce.

Manchester United wamekubaliana na klabu ya Fenerbahce kumsajili golikipa Altay Bayindir kwa kiasi cha Euro milioni 7 ambapo mpaka sasa golikipa huyo amekamilisha vipimo vya kwanza vya kwajili ya kujiunga na mashetani hao wekundu.

Klabu ya Man United ilihitaji golikipa mwingine kwakua golikipa wake namba mbili klabuni hapo Tom Heaton amepata majeraha na atakaa nje ya uwanja kwa kipindi fulani, Huku Dean Henderson akihitaji kuondoka klabuni hapo na kuelekea klabu nyingine ambayo atapata nafasi ya kucheza.

Klabu ya Man United kwasasa itakua na magolikipa wawili ambao watakua wapo fiti kwajili ya kucheza ambao ni Altay Bayindir kutoka Fenerbahce na golikipa namba moja wa klabu hiyo Andre Onana huku Tom Heaton yeye atakua nje kwa muda kidogo.

Klabu ya Fenerbahce wao wamehakikisha baada ya kumuuza golikipa wao kwenda klabu ya Manchester United wanasajili golikipa ambaye ataweza kuziba nafasi ya Bayindir, Kwani wameshakamilisha usajili wa golikipa namba moja wa timu ya taifa ya Croatia aliyekua anakipiga klabu ya Dinamo Zagreb Dominik Livakovic.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live