Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yakamilisha dili la Malacia, yahamishia nguvu kwa De Jong wa Barcelona

Skysports Erik Ten Hag Man Utd 5824426 1024x576 Malacia

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KLABU ya Manchester United imekamilisha dili la kumsajili mlinzi kutoka klabu ya Feyenoord ya nchini Uholanzi Tyrell Malacia kwa ada ya paundi milioni 12.9 ambayo inatarajiwa kupanda hadi kufikia paundi milioni 14.6 kwa kipindi cha miaka mine (4) huku kukiwa na kipengele cha kuongeza mkataba kwa mwaka mmoja zaidi.

Malacia alikuwa akigombaniwa na vilabu mbalimbali barani Ulaya vikiwemo Totenham Hotspurs.

Malacia mwenye umri wa miaka 22 anatajwa kuwa pendekezo la kocha mkuu wa klabua hiyo Erik Ten Hag ambaye amemfutailia kwa karibu tangu akiwa nchini Uholanzi.

Malacia anachangia wakala HCM Sports Management pamoja na kiungo raia wa Uholanzi Frenkie De Jong wa Barcelona ambaye naye anatajwa kukaribia kujiunga na mashetani wekundu wa Old Trafford.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live