Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yagawana point na Bournemouth

IMG 9805.jpeg Man United yagawana point na Bournemouth

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Manchester United imetoa sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji, AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Jana Uwanja wa Vitality mjini Bournemouth, Dorset.

Mabao yote ya Manchester United yamefungwa na kiungo Mreno, Bruno Fernandes dakika ya 31 na la penalti dakika ya 65, wakati ya AFC Bournemouth yamefungwa na mshambuliaji Muingereza, Dominic Solanke dakika ya 16 na Mholanzi, Justin Dean Kluivert dakika ya 36.

Kwa matokeo hayo, Manchester United inafikisha pointi 50 nafasi ya saba, wakati AFC Bournemouth inafikisha pointi 42 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 32.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live