Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yafunga mwaka kibabe, Yaichapa Burnley 3

B68C130A 327A 4A74 B119 A1FA28D385D4.jpeg Furaha ya Ushindi

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashetani wekundu, Manchester United wamefunga mwaka kibabe baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Old Trafford.

Mabao ya Manchester United yamefungwa na Scott McTominay dakika ya nane, Ben Mee aliyejifunga dakika ya 27 katika harakati za kuokoa krosi ya Jadon Sancho na Cristiano Ronaldo aliyekamilishwa shangwe za ushindi dakika ya 35.

Kwa ushindi huo, Manchester United ya kocha Mjerumani, Ralf Rangnick inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 18 na kusogea nafasi ya sita, wakati Burnley inabaki na pointi zake 11 za mechi 16 sasa katika nafasi ya 18.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live