Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United yaanza kwa kichapo

Man United Brighton Man United wachezea kichapo

Sun, 7 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United imeanza vibaya msimu mpya wa Premier League 2022/23 baada ya kufungwa magoli 2-1 katika mchezo dhidi ya Brighton kwenye Uwanja wa Old Trafford, leo Agosti 7, 2022.

Mabao yote mawili ya Brighton yamefungwa na Paschal Gross dakika ya 30 na dakika ya 39 huku bao la Man United likifungwa na Alexis McAllister dakika ya 68 baada ya kujifunga baada ya kipa Robert Sanchez kuushika mpira akiwa katika shinikizo za Harry Maguire.

Mchezo huo ni wa kwanza wa kiushindani kwa Kocha Erik ten Hag tangu aanze kuifundisha #ManUtd, ambapo pia alimtumia Cristiano Ronaldo katika kipindi cha pili.

Hatahivyo United ilizidiwa nguvu na timu ya Graham Porter katika safu zote katika kipindi cha kwanza .

Katika mechi tisa dhidi ya Man United, Brighton ilikuwa imefanikiwa kupata sare, hivyobasi ushindi huo ulikuwa wa kihistoria.

Kwa kocha Ten Hag , kulimaanisha kuanza vibaya kama mwenzake wa Uholanzi Louis van Gaal, ambaye alipoteza maechi yake ya kwanza kwa magoli hayohayonyumbani dhidi ya Swansea 2014.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live