Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United watumia nguvu ya pesa kuwakutanisha Kane, Rashford OT

Kane X Rashford Man United watumia nguvu ya pesa kuwakutanisha Kane, Rashford OT

Fri, 28 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United inataka kuwafanya Marcus Rashford na Harry Kane mshahara wa kibabe zaidi, Pauni 600,000 kwa wiki ili wawili hao wakawe pacha hatari katika kuisogeza timu hiyo kwenye ubingwa wa Ligi Kuu England.

Huo ndio mpango wa mabosi wa Old Trafford wakitaka kutumia fursa ya kufanya hovyo kwa Tottenham ili kumnasa straika huyo, Kane.

Kipa David de Gea ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Pauni 375,000 kwa wiki, lakini Mhispaniola huyo mwenye umri wa miaka 32, mkataba wake utakwisha mwisho wa msimu huu na dili lake jipya mshahara wake utashika hadi Pauni 200,000 kwa wiki.

Straika Rashford, 25, atakuwa amebakiza miezi 12 zaidi kwenye mkataba wake, ambapo dili jipya litafanya mshahara wake upande kutoka Pauni 200,000 hadi Pauni 300,000 kwa wiki.

Kane analipwa Pauni 200,000 kwa wiki huko Spurs, lakini kama atatua Man United watamwongeza Pauni 100,000 na hivyo atakuwa analipwa Pauni 300,000 kwa wiki.

Kane atafikisha umri wa miaka 30, Julai mwaka huu, lakini kuwa naye kwenye timu ni kujihakikishia mabao ya kutosha, hivyo kama atacheza pacha na Rashford kocha Erik ten Hag atakuwa na uhakika wa kikosi chake kuwa na fowadi ya kutisha.

Man United haijashinda ubingwa wa Ligi Kuu England tangu mwaka 2013, hivyo wanaamini kama watamchukua Kane kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi watakuwa kwenye nafasi kubwa ya kupambania ubingwa wa ligi hiyo msimu ujao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live