Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United watoa taarifa rasmi sakata la Anthony

Anthony Scandal Mhakamani Man United watoa taarifa rasmi sakata la Anthony

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchester United imetoa taarifa kuhusu mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Antony ambaye anatuhumiwa na unyanyasaji wa kijinsia kwa mpenzi wake.

Manchester United imeleeza inatambua tuhuma hizo na ikieleza pia inapisha uchunguzi wa polisi kwa kipindi na haitatoa maoni zaidi kipindi hichi ambacho polisi wanafanya uchunguzi.

Antony anatuhumiwa kumfanyia fujo mpenzi wake ambaye ni mama mtoto wake, Huku vyombo vinavyohusika vikiwa vinafanya kazi yake mpaka wakati huu jambo ambalo linaiweka Man United kwenye wakati mgumu.

Klabu ya Man United wamesema kua suala hilo wanalichukulia kwa uzito mkubwa kwa kuzingatia athari za madai hayo na kusema ripoti itakayofuata itakua kwa waathiriwa.manchester unitedHii ni mara ya pili ndani ya miaka miwili wachezaji wa Manchester United wanakumbwa na tuhuma za namna hii, Kwani mwaka 2021 mchezaji Mason Greenwood alikumbwa na tuhuma ya namna hii na sasa imehamia kwa mchezaji Antony.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live