Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United watembezewa kichapo kikali EPL

Palace Vs United Wachezaji wa Crystal Palace wakishangilia goli mchezo wao na Man United

Tue, 7 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Crystal Palace wameipa kipigo kizito Manchester United cha mabao 4-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumatatu Uwanja wa Selhurst Park Jijini London.

Kiungo wa umri wa miaka 22, Michael Akpovie Olise amefunga mabao mawili dakika ya 12 na 66, huku mabao mengine yakifungwa na Mfaransa mwenzake, mshambuliaji Jean-Philippe Mateta (26) dakika ya 58 na beki Muingereza, Tyrick Kwon Mitchell (24) dakika ya 66.

Kwa ushindi huo, Crystal Palace wanafikisha pointi 43 katika mchezo wa 36 nafasi ya 14, wakati Manchester United wanabaki na pointi zao 54 za mechi 35 nafasi ya nane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live