Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United wasubiri ripoti ya mwanasheria sakata la Ronaldo

Cristiano Ronaldo Erik Ten Hag 3 169.jpeg Man United wasubiri ripoti ya mwanasheria sakata la Ronaldo

Tue, 15 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchester United itapata ushauri wa kisheria kwanza kabla ya kufanya chochote kuhusiana na mahojiano aliyoyafanya Cristiano Ronaldo na Mtangazaji maarufu wa Uingereza Piers Morgan.

Manchester United wanaweza kufikiria kuvunja mkataba wa fowadi huyo wa Ureno Cristiano Ronaldo kufuatia mahojiano yake na Piers Morgan lakini watasubiri hadi watakaposikia mahojiano kamili kabla ya kufanya uamuzi kuhusu mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37.

Ronaldo anaweza kwenda Chelsea baada ya fowadi huyo kuhusishwa na kuhamia Stamford Bridge majira ya joto lakini iliripotiwa kuzuiwa na meneja wa wakati huo Thomas Tuchel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live