Klabu ya Manchester United inaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Brentford na England, Ivan Benjamin Elijah Toney katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi mbele ya timu nyingi zilizokuwa zikimhitaji.
Arsenal imeripotiwa kuwa haina mpango wa kutoa kiasi cha pesa kinachohitajiwa na Brentford ili kumuuza fundi huyu, wakati Chelsea ikidaiwa kuwa kwenye harakati za kutafuta mshambuliaji mwingine.
Hiyo inaiacha Man United yenyewe kwenye mchakato huo na kuna uwezekano ikakamilisha mchakato wa kumsajili mara tu baada ya dirisha lijalo kufunguliwa ingawa itahitaji kuuza baadhi ya mastaa.
Toney mwenye umri wa miaka 27, mkataba wake unamalizika mwaka 2025 na anadaiwa kuuzwa kwa zaidi ya Pauni 70 milioni.
Staa huyu wa England tangu apande ligi Kuu na Brentford mwaka 2021, amefunga mabao 34 kwenye mechi 68 za ligi hiyo pendwa.