Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United warudi Epl na ushindi

United Vs Nottigham Man United warudi Epl na ushindi

Wed, 28 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji Manchester United wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Nottingham Forest katika mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.

Mabao ya Man United yamefungwa na Marcus Rashford dakika ya 19, Anthony Martial dakika ya 22 na Fred dakika ya 87.

Kwa ushindi huo kikosi cha kocha Mholanzi Erik ten Hag kinafakisha pointi 29 katika mchezo wa 15, ingawa kinabaki nafasi ya tano kikizidiwa pointi moja Tottenham Hotspur ambayo pia imecheza mechi moja zaidi, wakati Nottingham Forest wanabaki na pointi zao 13 za mechi 16 nafasi ya 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live