Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United wapigwa bao 4 na Bayern Munich UEFA

IMG 5787 Bayern Vs United.jpeg Bayern Munich walishinda kwa magoli 4-3

Thu, 21 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Manchester United imeanza vibaya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchapwa mabao 4-3 na wenyeji, Bayern Munich katika mchezo wa Kundi A usiku wa Jana Uwanja wa Allianz Arena Jijini Múnich nchini Ujerumani.

Mabao ya Bayern Munich yamefungwa na Leroy Sané dakika ya 28, Serge Gnabry dakika ya 32, Harry Kane kwa penalti dakika ya 53 na Mathys Henri Tel dakika ya 90 na ushei.

Kwa upande wao, Manchester United mabao yao yamefungwa na Rasmus Højlund dakika ya 49 na Carlos Henrique Casemiro dakika ya 88 na 90.

Mchezo mwingine wa Kundi A, wenyeji Galatasaray walitoka sare ya 2-2 na FC Copenhagen Uwanja wa Rams Global mjini İstanbul nchini Uturuki.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live