Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United wapigwa Faini na FA

Man United Fine Man United wapigwa Faini na FA

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Manchester United imepigwa faini na shirikisho la soka nchini England kutokana na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu katika michezo yao miwili ya ligi kuu nchini England.

Klabu hiyo imekumbwa na faini hiyo kutokana na madai yanayowakabili katika michezo miwili ya ligi kuu nchini England kati ya Chelsea na klabu ya Newcastle michezo yote ikipigwa ndani ya mwezi wa kumi na kumalizika kwa suluhu.

Man United ilishindwa kuwazuia wachezaji wake wasiwazonge waamuzi katika tukio la kukataliwa goli kwenye mchezo dhidi ya Newcastle huku katika mechi ya Chelsea wachezaji wa klabu hiyo walionekana kumzonga mwamuzi.

Baada ya adhabu hiyo kutolewa klabu ya Manchester United imekiri makosa yaliyoorodheshwa na kuahidi watahakikisha wachezaji wanaweza kujiongoza na kufata kanuni zilizowekwa ili kuepusha sintofahamu na adhabu kama hizo.

Klabu yeyote ambayo imekua ikivunja kanuni katika ligi kuu ya Uingereza shirikisho la mpira chini humo Fa hua wanasimamia utaratibu na kutoa adhabu kwa klabu yeyote ambayo hua inakiuka kanuni zilizowekwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live