Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United wanamtaka Kalvin Phillips

Kalvin Phillips Hag Kalvin Phillips.

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kalvin Phillips yuko juu ya orodha ya ununuzi ya Manchester United majira ya joto, mara baada ya Manchester City kumuonesha mlango wa kutokea.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza anaelekea kuondoka Etihad huku Pep Guardiola juma lililopita akikiri kwamba haoni nafasi ya kumtumia katika timu yake ya City.

Lakini, wadadisi wa mambo wanaeleza kuwa Kocha Mkuu wa Man Utd Erik Ten Hag ni shabiki mkubwa na kwamba Phillips ndiye anayefaa kwa mwelekeo mpya anaotaka kuelekea.

Chanzo hicho kilisema: “United wanaangalia hali ya Phillips kwa uangalifu sana. Ana uwezekano wa kwenda nje kwa mkopo Januari 2024, lakini atatafuta usajili Wa kudumu.

“Yeye ni shabiki wa jinsi Phillips anavyocheza, na anadhani mtindo wake unafaa kabisa kwa United na kwa falsafa anayojaribu kuingiza kwenye timu.

“Pamoja na hayo, wawekezaji wapya wanataka klabu kuwekeza nguvu katika kujenga kikosi na kuendeleza wachezaji wa Kiingereza, na Phillips bado anasalia kuwa mmoja wa wachezaji bora wa Kiingereza katika Ligi Kuu.

“Haitakuwa mara ya kwanza kwa mchezaji kuhama kutoka City kwenda United, lakini huwa na utata.”

Chanzo hicho kiliongeza: “Kuna hisia kwamba Guardiola angesimama katika njia ya Phillips. Uhamisho wa kwenda City haujafanikiwa na Guardiola anatamani hali hiyo kutatuliwa haraka iwezekanavyo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live