Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United wamwambia Rashford "Ukitaka sepa"

Manchester United Vs West Ham Marcus Rashford Sends Red Devils 1024x576 Marcus Rashford

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United imesema kwamba haitamzuia Marcus Rashford endapo kama mshambuliaji huyo atahitaji kubadili timu.

Staa huyo wa kimataifa wa England alikuwa na msimu wa hovyo kwelikweli kwa 2023-24, ambapo alifunga mabao manane tu katika mechi 43.

Kiwango hicho kilimfanya akose nafasi ya kuwapo kwenye kikosi cha Three Lions kilichokwenda kwenye fainali za Euro 2024, ambako kocha Gareth Southgate alijaribu kuteua wachezaji waliofanya vizuri kwenye klabu zao.

Man United iliweka orodha ya mastaa saba ambao haina mpango kabisa wa kuwauza kwenye dirisha hili na Rashford hayumo kwenye orodha hiyo.

Kipa Andre Onana amejumuishwa kwenye orodha hiyo sambamba na Diogo Dalot, Lisandro Martinez, Kobbie Mainoo, Alejandro Garnacho, Amad Diallo na Rasmus Hojlund.

Kwa maana hiyo, hata nahodha Bruno Fernandes hajawekwa kwenye orodha ya wachezaji ambao Man United itatumia nguvu zao zote kuwazuia endapo kama watataka kuondoka kwenye timu hiyo.

Kumekuwa na ripoti kwamba kuondoka Old Trafford pengine ni kitu kinachoweza kupewa nafasi na Rashford ili kwenda kucheza kwenye mazingira mapya yanayoweza kuwa na hamasa kubwa kwake kurudi kwenye viwango bora na kurejea kuichezea timu ya taifa.

Lakini, kinachoelezwa ni kwamba Rashford, 26, anataka kubaki na kugombea nafasi yake Old Trafford. Alifunga mabao 30 katika msimu wa 2022-23, katika msimu wa kwanza wa kocha Erik ten Hag na uamuzi wa mabosi wa timu hiyo kubaki na Mdachi huyo wanaamini atamrudisha kwenye ubora wake mchezaji huyo ambaye ni zao la kutoka kwenye akademia ya klabu hiyo.

Mkataba wa sasa Rashford utafika tamati majira ya kiangazi 2028, hivyo bado ana muda wa kutosha wa kubadilisha hali ya mambo kwenye kikosi hicho kabla ya kufikiria kutimka na kwenda kuanza maisha mapya kwingineko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live