Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United waikimbia Liverpool Top Four EPL

WhatsApp Image 2023 05 14 At 11.jpeg Wachezaji wa Man United wakishangilia ushindi wa jana

Sun, 14 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashetani wekundu, Manchester United wameibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.

Mabao ya Man United yamefungwa na Anthony Martial dakika ya 32 na Alejandro Garnacho dakika ya 90 na ushei na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 66, ingawa wanabaki nafasi ya nne, wakizidiwa tu wastani wa mabao wa Newcastle United baada ya wote kucheza mechi 35.

Kwa upande wao Wolverhampton Wanderers baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 40 za mechi 36 nafasi ya 13.

Ushindi huo wa Man United ni kama wanawakimbia wapinzani wao wa karibu Timu ya Liverpool ambao wanapambana kuingia Top Four.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live