Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United waichapa Liverpool na kutinga Nusu Fainali FA

Man U Beat Liverpool Man United waichapa Liverpool na kutinga Nusu Fainali FA

Sun, 17 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United imeshinda kibabe sana moja ya mechi ngumu kabisa kwenye Kombe la FA baada ya kuichapa Liverpool 4-3 katika mchezo uliochezwa kwa dakika 120 uwanjani Old Trafford.

Kikosi hicho cha Erik ten Hag kilitangulia kwa bao la Scott McTominay, Liverpool ikafunga mara mbili ndani ya dakika tatu na kuongoza 2-1 kabla ya mapumziko.

Man United ikionekana kama imekata tamaa ya kuwamo kwenye taji lolote msimu huu, Mbrazili Antony alirudisha matumaini baada ya kusawazisha na kufanya matokeo yawe 2-2 kulazimisha mechi hiyo kuingia kwenye dakika 30 za nyongeza.

Kasheshe jingine likatokea kwa Man United baada Harvey Elliott kujifungia bao jingine Liverpool, lakini Marcus Rashford alisawazisha kabla Amad Diallo kufunga bao la nne kwenye dakika 120 na hivyo Man United kupinga nusu fainali ya Kombe la FA kibabe.

Vikosi, Man United: Onana, Wan-Bissaka, Lindelof, Varane, Dalot, Mainoo, McTominay, Fernandes, Garnacho, Rashford, Hojlund.

Liverpool: Kelleher, Gomez, Quansah, Van Dijk, Robertson, Szoboszlai, Endo, Mac Allister, Salah, Diaz, Nunez.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live