Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United wachukua pointi 3 dakika za majeruhi

Scott Mac Tominay Vs Berntford Man United wachukua pointi 3 dakika za majeruhi

Sun, 8 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wenyeji, Manchester United wametoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Brentford FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England jana Jumamosi Uwanja wa Old Trafford Jijini Manchester.

Kiungo Mdenmark, Mathias Jensen alianza kuifungia Brentford FC dakika ya 26, kabla ya kiungo Mscotland, Scott McTominay kuifungia mabao mawili Manchester United dakika za nyongeza baada ya kutimia dakika 90 za kawaida (90'+3 na 90'+7).

Kwa ushindi huo, Manchester United inafikisha pointi 12 na kusogea nafasi ya tisa, wakati Brentford FC inabaki na pointi zake saba nafasi ya 14 baada ya wote kucheza mechi nane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live