Manchester United imeitandika Leicester City bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu England mtanange uliopigwa dimba la King Power Jana usiku ukiwa ni ushindi wa tatu mfululizo kwa kocha Erik ten Hag.
Bao pekee ambalo limeweka utofauti kwenye mechi hiyo limefungwa winga wa kimataifa wa England Jadon Sancho akimalizia shambulizi la kujibu lililoanzishwa na Diogo Dalot kwenda kwa Bruno Fernandes kisha kumpasia Marcus Rashford kabla ya Sancho kuhitimisha kwa bao rahisi.
Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kufikisha pointi tisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu wakiwa nafasi ya tano alama moja dhidi ya Liverpool nafasi ya sita alama sita pungufu ya vinara Arsenal.
Walianza Liverpool kufungwa wakaja Southampton kisha Leicester City kwenye mechi tatu ambazo Manchester United wameshinda tofauti na zile mbili za awali ambazo walifungwa ya Brentford na Brighton.