Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man United kuuzwa imebaki hadithi

Skynews Old Trafford Manchester United 6059826 Klabu ya Manchester United

Sun, 12 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Habari ndo hiyo. Manchester United huenda ikaondoshwa sokoni na mpango wa kupigwa bei ukafutwa kabisa.

Na badala yake, wamiliki wa klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford, familia ya Glazer wakaja na mpango mwingine wa kuzalisha pesa kutoka kwa mashabiki wao na si mambo ya ndani ya uwanja.

Licha ya kukubali kukutana na walionyesha dhamira ya kuinunua klabu hiyo, bilionea Sir Jim Ratcliffe na kiongozi wa Qatari, Sheikh Jassim bin Hamad al-Thani kujadili biashara ya kuiuza klabu hiyo, kuna mipango mingine inayoweza kutumika ili kuachana na mpango wa Man United kuuzwa jumla jumla.

Kinachoelezwa kwa sasa hakuna dalili ya wanaotaka kununua klabu hiyo ya Man United wakaweka dau linalotakiwa na familia ya Glazer la Pauni 6 bilioni. Siku za karibuni kulikuwa na maelezo kwamba ndugu wa familia ya Glazer kuwapo na mpango wa wanandugu Joel na Avram kutaka kununua hisa za ndugu zao ili wao ndio wawe wamiliki wa jumla. Hilo limedaiwa si la kweli.

Kampuni ya Raine Group, iliyoteuliwa na familia ya Glazer kusimamia mchakato wa kupigwa bei kwa Man United wamepanga kufanya kuweka mambo sawa baadaye mwaka huu, hivyo ishu hiyo uamuzi wa mwisho utakuwa bado haujafikiwa.

Mpango wa kuinunua jumla Man United ni wa bilionea Sheikh Jassim, mmoja wa watu wa familia ya kifalme huko Qatari. Lakini, jambo jingine linalofikiriwa ni la kufuata wazo la kampuni ya Ineos ya bilionea Ratcliffe ya kutaka kununua hisa asilimia 69 na si kuinunua timu nzima, huku hisi zilizobaki zitatolewa fursa kwa wawekezaji wengine kuzimiliki.

Lakini, mpango mwingine unaoripotiwa kupewa nafasi kubwa ni wa kutumia pesa ya nje, ambapo kuna kampuni nne za Kimarekani zitatengeneza mchakato mahususi wa kuuza bidhaa mbalimbali za klabu hizo kidigitali ili kuzaliwa pesa.

Kwenye mpango huo, familia ya Glazer itaungana na taasisi moja ya fedha maarufu ya Ares Management iliyopo Los Angeles, ambayo ina utajiri wa Pauni 246 biioni kuna na mpango huo mpya wa kutengeneza pesa nje ya klabu. Taasisi hiyo kitu ambacho itafanya ni kutafuta fursa ya kuingiza pesa kiditali kwa kuuza bidhaa mbalimbali za klabu ya Man United kama vile video za michezo ya kompyuta, jezi na bidhaa nyingine, ambazo zitauzwa mtandao ili kupata pesa nje ya kinachotokea uwanjani.

Mpango huo ukikaa vizuri utafuta kabisa ishu ya familia hiyo kutaka kuipiga bei jumla Man United. Hata hivyo, kwa sasa mtazamo wa walio wengi ni kwamba Man United itauzwa jumla.

Hata hivyo, mpango wa mabosi wote walionyesha dhamira ya kuinunua klabu hiyo wamepanga kukamilisha mchakato hadi kufikia Mei 31 ili kupata nafasi muhimu ya kushiriki kwenye usajili wa dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kunasa mastaa wapya.

Kwa mujibu wa ripoti mpya zinadai kwamba Raine imedhamiria kuweka mchakato mzuri kabisa kwa ajili ya wenye dhamira ya kuinunua klabu ya Man United kufichua ofa zao ili kukimbizana na muda uliopangwa kabla ya kufikiwa kwa uamuzi wa mwisho.

Mchakato huo utaweka wazi mambo yote ya kisheria, kodi, mali, mikataba na taarifa za wachezaji kabla ya wawekezaji wapya wanaotaka kuwekeza kwenye klabu hiyo hawajaweka pesa mezani kulingana na thamani ya klabu hiyo.

Mpango huo mpya utawekwa ili kuwafanya wanaotaka kununua klabu hiyo kufahamu thamani halisi ya Man United hasa kutokana na kipindi hiki ambacho familia ya Glazer haipo tayari kushusha bei, huku kwa mujibu wa soko la hisa la New York Man United inathaminishwa kuwa na thamani inayozidi Pauni 3 bilioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live